05 April, 2015

matokeo ya Borussia Dortmund vs Bayern Munich hapa


Wikiendi mbili zilizopita tulishuhudia vilabu mahasimu wa ligi za England Manchester UTD vs Liverpool na FC Barcelona va Real Madrid wakiumana – jana ilikuwa zamu ya Bundesliga – ambapo Borussia Dortmund waliwakaribisha wapinzani wao Bayern Munich katika dimba la Siguna Iduna Park.
Mchezo huo uliomalizika muda mfupi uliopita umeshuhudia Bayern wakipata ushindi mgumu wa goli 1-0 dhidi ya vijana wa Jurgen Klopp.
Robert Lewandoski mchezaji wa zamani wa Dortmund ndio aliyepeleka kilio kwa mashabiki wa timu yake ya zamani – baada ya kuunganisha kwa kichwa mpira uliokolewa na kipa wa Dortmund mapema katika kipindi cha kwanza.
Kwa matokeo hayo Bayern Munich wanaendelea kuongoza msimamo wa ligi kuu ya Ujerumani.
                         Matokeo mengine ya Bundesliga
 

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...