NIPASHE
Askofu Gwajima anatakiwa kuripoti muda
wowote kuanzia leo katika Hospitali ya TMJ kwa uchunguzi zaidi baada ya
kuisha kwa muda ambao alipewa kwa ajili ya kupumzika.
“Tulimpa
muda wa wiki moja, hadi sasa muda umekwisha, hivyo wakati wowote
anatakiwa kuripoti Hospitalini ili kuangaliwa maendeleo ya hali yake na
kama haijaimarika, tutamchunguza zaidi”—Dk. Fortunatus Mazigo, daktari ambaye anamtibu Askofu huyo.
Daktari huyo amesema hawezi kuuzungumzia
ugonjwa ambao anaumwa Askofu huyo kutokana na maadili ya kazi yake, ila
akipata ruhusa kutoka kwa mhusika mwenyewe atafanya hivyo.
MTANZANIA
Ndoa ya Dk. Mengi ana Jacquiline Ntuyabaliwe ambayo ilifungwa kwa siri Mauritius ana kuhudhuriwa na marafiki wachache takribani 50 imezua gumzo.
Safari ya wawili hao kuelekea uchumba
ilianza Desemba mwaka 2014 ambapo walivalishana pete za uchumba katika
sherehe za kumbukumbu ya kuazaliwa ya Jacquiline iliyofanyika Dubai.
Rafiki wa karibu na Jacquiline, Nancy Sumari aliweka picha katika ukurasa wake wa Instagram ikimuonesha Jacquiline akirusha juu maua pamoja na rafiki zake akiwemo Faraja Kota, Nasreen Kareem na Sophia Byanaku.
Mengi na Jacquiline tayari wana watoto mapacha ambao nao pia walihudhuria ndoa ya wazazi wao.
MWANANCHI
Familia ya Diwani wa viti Maalum Mkoa wa Geita, Helena Mahona
imevamiwa na kushambuliwa na nyuki ambao wamejeruhi mama mmoja na
watoto wawili na kusababisha kifo cha mtu mmoja ambaye ni shangazi wa
Diwani huyo.
Ofisa Mtendaji wa Kijiji hicho, Joseph Majebele amesema alikuwa mbali na eneo hilo lakini akapewa taarifa ya kutokea kwa tukio hilo kwa njia ya simu na watu walioshuhudia.
Kamanda wa Polisi Geita, Peter Kakamba
amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa marehemu alifariki
hapo hapo kwenye tukio huku majeruhi wakikimbizwa Hospitai na hali zao
zinaendelea vizuri.
No comments:
Post a Comment