Kiongozi wa mashtaka katika mahakama ya kimataifa ya Jinai ICC, iliyoko
the Hague Uholanzi, Fatou Bensouda, amesema kuwa kundi la wapiganaji la
Islamic State,
limetekeleza uhalifu wa hali na ukatili mkubwa nchini Syria na Iraq.
Bensouda
amesema uhalifu huo unahatarisha amani, usalama sio wa eneo hilo tu
bali dunia kwa ujumla, lakini amekariri kuwa Iraq na Syria sio wanachama
wa mahakama hiyo.
Wengi wa wapiganaji wa kundi hilo ni raia wa Kigeni ndio maana mwendesha mashtaka huyo mkuu anasema hana budi ila kusalimu amri.
Maelfu
ya wapiganaji wa kigeni wamejiunga na wapiganaji wa ISIS, wakiwemo raia
wa Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Ubelgiji, Australia na Tunisia.
Licha
ya kuwa nchi hizi ni wanachama wa mahakama ya ICC, Bensouda anasema
kuwa kundi hilo la ISIS linaongozwa na raia wa Iraq na Syria.
Na
kwa sababu nchi hizo sio wanachama wa ICC, Bi Bensouda amesema kuwa
uwezekano wa kuchunguza wale waliohusika zaidi chini ya uongoza wa ICC
ni finyu kabisa.
Aidha ametoa wito kwa mataifa wanachama kutafuta mbinu za kuwawajibisha wale waliohusika.
Baraza
la Usalama la Umoja wa mataifa halina mamlaka kuwasilisha kesi katika
mahakama hiyo kuhusiana na hali ilivyo nchini Iraq na Syria.
Ameongeza
kuwa kuwa uhalifu unaondelea kutekelezwa nchi humo unakiuka maadili
yote ya kibinadam na ni sharti waliohusika kufunguliwa mashtaka.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7
KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...
-
C9 Records presents STAR by Foby!. Click DOWNLOAD button bellow to download this song.
-
John ana mke ambaye haoni uzuri wa kitu chochote anachofanya, akifika tu nyumbani mke wake huanza kumlalamika kuwa hela anayoacha nyumba...
-
Mboga za majani na matunda zimekuwa zikisisitizwa kwa sana na wataalamu wa afya hasa kwa wanawake wajawaziti kwani zimekuwa zikiongeza Damu...
No comments:
Post a Comment