27 April, 2015

ALIKIBA NI MOJA YA MWANAMUZIKI MZURI AMBAE ANA MANAGEMENT ILIYISHINDWA KUKABILI SOKO LA MUZIKI TZ?

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjkMC1Vxha6V3y7y2z7lLVwSOqNfWImLWF9-ko0pDQhEGHF9lYHdOSapMkNWAlFce2tFgCaU6GghfGV8yK8hrrN_vo4_M0sqjbjjfGD-AHuGF0Oqdus-9d_v12K3d2Lo_OI-ia7YYEHHt9N/s1600/ALI+KIBA+GETS+SHAVED.jpgNi ukweli ulio wazi kabisa Alikiba ni mmoja wa waimbaji/wanamuziki bora kabisa na mwenye kipaji cha aina yake hasa kuimba!
Ni wazi soko la muziki limebadilika sana na limekuwa na ushindani wa hali ya juu na pengine uwezo wa msanii unaweza usipimwe kwa kipaji chake bali uwezo wake wa kulikabili soko na kuendana na mahitaji ya soko la muziki! Na hapa kwenye mipango ndipo watu hushikana uchawi na kuanza kutuhumia ooh fulani ana bebwa ooh fulani anatumia nguvu za giza ..kumbe muda mwingine ni mipango tuu...
kuna jamaa wa futuhi husema "Mjini mipango.

Nami naamini soko hili hasa la sasa lina hitaji mipango na uthubutu wa hali ya juu kinyume na hapo soko litakushinda!

Alikiba ni mmoja ya wasanii wenye uwezo mkubwa sana na mwenye ushawishi sokoni lakini naamini ni mmoja wa wasanii mwenye management mbovu na iliyo choka kufikiri kabisa!
Management ya Alikiba haijawai kumbadilisha alikiba wala kumfanya Alikiba kuwa msanii mkubwa kama matarajio ya watu!Wakati Alikiba anarudi nilitegemea atarudi huku akiwa amejiandaa kulikabili soko la muziki ambalo kwa sasa lina changamoto nyingi na halitegemei kipaji tuu!

Hivi management ya Alikiba haifahamu kuwa kwa sasa Video ina mtangaza msanii kuliko audio?
Hivi management ya Alikiba imeshindwa kumpandisha thamani Alikiba?
Hivi kweli Alikiba nae hadi sasa ana stahili kujumuishwa kwenye show zisizo na tija hasa zile zinazo onekana kabisa hazilipi?
Tangu Alikiba amerudi sijaona cha kipekee ambacho amerudi nacho kuweza kupambana na soko la muziki na ukweli ni kwamba Alikiba hakujipanga au kuna tatizo kubwa kwenye management yake!

Kusema kweli ni wazi ana hitaji kuitazama upya management yake pengine kuibadilisha kabisa maana haina tija kwakwe na ina mdanganya sana!
Hivi Alikiba na management yake wameshindwa kujua kuwa video inafanya wimbo huduma milele?

Pengine sio dhambi na sijawai kuhisi ni dhambi kuiga kwa wengine...kuanzia thamani ya show na kumbrand msanii na bila shaka mashabiki wa Alikiba wanatamani kuona Alikiba anaonekana kuwa ni msanii mkubwa si masikioni tuu bali hata machoni mwa watu..!

Watanzania pamoja na shida walizo nazo linapokuja swala la kutumia hela kwa burudani huwa wako tayari kabisa tatizo wasanii wetu wanashindwa kutumia fursa..kwakweli Alikiba ni msanii aliye shindwa kuchukua hela ambazo watanzania wanazo kwaajili yake na kipaji alicho nacho!

Nimeamua kuyasema haya kwasababu nimegundua kuna mambo Alikiba na management yake hawaambiwi kabisa na bila shaka wata jitazama upya kama kweli hii ndio thamani ya Alikiba tunaye msikia kila leo!

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...