Francis Paul Mawere |
Dhamira kuu ya kuanzisha blog hii ni kuijenga jamii inayo nizunguka na hasa vijana wenzangu ambao mara nyingi wameonekana wakipotea katika mambo yasiyo na tija.
Unaweza kuniuliza je ni kwa nini muda mwingi katika blog yako unaongelea maswala ya Burudani ya Muziki na ilhali umesema Blog yako ni kwa ajili ya kuijenga jamii?
Ukiniuliza swali la aina hii mimi nitakujibu kama ifuatavyo.
Muziki ni darasa tosha katika jamii yeyote ile hapa ulimwenguni. Hivyo kwa kulitambua hilo nitakua nmeweza kuifikia jamii kwa urahisi pasipo hata kutumia gharama kubwa kuwafikia walengwa.
Nilipo kua chuonio niliweza kuyaona matatizo meengi yanayoikumba jamii iliyo kuwa ikinizunguka kwa wakati ule hasa vijana weengi walio kuwa na matatizo mbali mbali kama vile ULEVI, ZINAA, UVIVU na mambo meengi lukuki na tangu hapo ndipo nilipo amua kuifungua blog hii ya MTOKAMBALI kwa ajili ya vijana wenzangu.
Naamini kabisa tutaburudika na tutaelimika kama utakubali kuabadili mtazamo wako mbovu na fikra zako potofu juu ya maisha haya,Niliwahi kuandika Makala zaidi ya Tatu humu humu ndani ambazi ni KIJANA BADILI MTAZAMO WAKO NA JENGA MAISHA BORA, Sababu kuu nne ni kwa nini Unashindwa kufuata ndoto zako leo , na Furaha ya kweli inaletwa na wewe mwenyewe .
Zaidi ya yote nliigusa jamii kwa ujumla wake kwa maana kwamba niliwahi kiuzungumzia jamii katika Elimu, siasa na Michezo. Unaweza kusoma makala zangu kama vile Elimu ya Tanzania yenye mfumu wakikoloni na Misitu yetu Tanzania Tuna Faidikaje Nayo. Zote hizo nimzungumzia jamii na mambo yake kiujumla.
Kwa nini nakuambia chagua MTOKAMBALI.
1. Utahabarika na kuelimika
2.Utapata kufahamu yale mambo ambayo hukuyajua toka mwanzoni.
3.Uta hamasika
4. Fikra chanya na mchanganuo wa mambo.
5.Hakuna Upendeleo.
Tambua!
Mimi kama Francis Mawere ni kijana mdogo sana ila kwa kua nilikukia katika jamii na familia iyo-kuwa na misingi bora leo hii naweza kusimama mahala nikamshauri mtu mzima na alonipita kiumri, kiakili, kimwili, na kimali na hata akapata kunisikiliza.
Napenda sana kukutia moyo ewe kijana mwenzangu maana nafahamu fika kuwa changamoto za maisha ni nyingi mno ila yakupasa kupambana kuime.
Naamini!
Kufanikiwa katika maisha siyo kuota tuu ndoto kila siku yakua iko siku utapata, laa hasha... Muda ulio nao wewe ni mchache mmno, hivyo unapata picha kwamba, ule Muda wa kuishi maisha ya ndoto zako ni leo na sio kesho tena maana hakuna anaye ijua kesho.
No comments:
Post a Comment