18 March, 2016

Sababu kuu nne ni kwa nini Unashindwa kufuata ndoto zako leo

chase your dreams, why people don't chase their dreams
Je umewahi kujisikia vibaya ama kua katika hali fulalini yakuonyesha kua umekwama katika maisha ambayo hayakupendezi ama sio yale uliokua ikitamani kuishi?
Kama jibu ni NDIO basi kaa nami hapa maana unastahili kuwa hapa leo na nmewahi kua katika hali kama ulio nayo leo. Embu twende pamoja.
Kabla ya yote ningependa uitazame hii video Hapo chini ambayo ni ISPARATION VIDEO kutoka kwa mmoja kati ya watu waliofanikiwa sababu tuu waliweza kufuata ndoto zao Ni matumaini yangu umepata kitu ama vp? Sasa tuweke utani pembeni na kuweza kuingia moja kwa moja katika kile tunacho kiita MAADUI katika maisha yako na unashindwa kufikia pale ulipotamani kufikia

HAWA HAPA MAADUI ZAKO

1: HOFU

Adui yako namba moja ni Hofu. Hofu ya kutokujulikana, Hofu ya kushindwa, hofu ya kupnekana kua unachokifanya ni ujinga, hofu ya kueleza hisia zako. 
Imekuchukua muda mrefu kujitambua kua umejifunga mwenyewe katika gereza la HOFU na hata ukashindwa kufikia malengo yako na hasa kupitia ndoto zako.

 Ni nini hasa Unachokitaka katika masha yako?
Hi ni swali moja ambalo unapaswa kuwa nalo katika kichwa chako kila uamkapo, utembeapo na ulalapo. Iko hivi, huwezi kamwe kufanikiwa katika masha pasipo kufamu ni nini unachokitaka na utafanya nini ili uweze kufanikiwa katika Takwa hilo. Ndio kila mmoja anapaswa kuwa na hofu lakiniki hali hiyo iwe katika mambo kama ya kiimani mfano Hofu ya Mungu na hofu ya kutenda dhami na sii vinginevyo. Katika maisha yako Kamwe hofu ya Maisha isikuingie kamwe, Jiamini kua unaweza.

Ukweli ni kwamba una NDOTO KUBWA ila kuna kitu kinakuchoma na kukumaliza mwilini mwako na kitu hicho ni HOFU. Ni kweli usiopingika ya vijana wengi hatujiamini, tumekua tukifanya fanya mambo kwa HOFU ama kwa kutokujiamini na ndio maana wengi wetu tunaishia Katika kufeli kila jambo tunalokua tukifanya katika masha yetu.
Badili mfumo wa masha yako leo maana utaondokana na kifungo ulichonako leo. Fanya kweli ondoa HOFU jenga misingi thabiti ya maisha yako na DHAMIRIA MOYONI KUFANYA KWELI
 If you really want something, you will find a way.If you don’t, you’ll find an excuse.
 Hakuna aliewahi kujaribu kufanya kweli akaambulia patupu. Nikupatie mfano hai mmoja ambao kila mtu ameuona Fikiria Mark Zukernbag ambae ni mwanzilishi wa Facebook ambayo leo hii dunia nzima inaitumia angekua na Hofu ya kuanzasha mtandio huo eti kwa kua teyari walikuwepo wakina GOOGLE na wenzake leo hii ungeisiklia wapi FACEBOOK? sasa jifunze kitu hapo ndugu.
If you want big things out of life, you have to face your fears.And since that’s what I’ve always wanted, that’s what I’ve always done.
2: KUKATA TAMAA MAPEMA
  Huyu ni adui mkubwa nambari mbli ambae wengi wamekutana nae katika maisha yao. Wengi hukata tamaa mapema kabla ya kukaribia kileleni cha mafanikio yao.
Linganisha Maisha yako na Hadithi ya mapenzi: Ndo, fikiria ndoto yako kana kwamba ni sawa na mpenzi wako amabe umezama nae katika penzi zito na baada ya miezi machache mambo yakaenda vizuri na uko katika "Kipindi cha fungate" na baadae ukawa na shauku ya kumfuatila mpenzi wako na ndipo unaundua dosari nyingi juu ya mpenzi wako huyo. You get a bit bored, kitu ambacho ni kawaida katika mapenzi na baadae unaona kua ni umefanya chaguo ambalo sio sahihi na unaamua kuachana na mpenzi huyo.
Your dream, just like with love, unahitaji muda na bidii ili ndoto yako iitwe mafanikio. Sio raihisi kwa kweli maana kila muda utakua ukipata majaribu, rafiki zako watakua wakikukatisha tamaa lakini siyo kitu, cha msingi ni kutazama katika malengo yako uliyo jiwekea ili kufikia mafanikio yako.
   Mfano mzuri ni mimi pale nlipoamua kufungua blog hii wakati nikiwa chuoni, nilifanya kazi usiku na mchana lakini sikuona mafanikio yeyote na kutokana na nilikua na shahuku yakufanya kweli kupitia blog hii, sikufa moyo bali nilizidi kujituma na hata mara nyingine nilikua nikipunguza muda wangu wa masomo ili tuu niweze kuifikisha blog hii panapostahili,
    Sikufa moyo japo nilipata majaribu mengi na kweli kuna wakati nlitaka kukata tamaa lakini Shauku ya mafanikio nliyokua nayo ilinifanya kujituma zaidi na kwa kweli Matunda nmeyaona japo bado Sio kama nlivyodhamiria,
Mtu pekee unaeweza kujilingasha nae ni ..... WEWE.
Je umeona afadhali ukijilingasha na nyuma ulipotoka? kama jibu ni NDIO you can relax and keep on working harder than ever. Hutoweza kukosea kamwe.
And what if something actually does goes wrong? Admit the defeat, analyze your mistake, get back up, and keep trying.
Successful people are not necessarily geniuses; they are those who never gave up. The ones who see an obstacle as an opportunity.
3: KUSUBIRIA MUDA SAHIHI.
 This reason is what I call the “black dress excuse” Linafiti katika kila tukio/Sherehe. Ilinichikua muda mwingi kuanza kuamini. Kuna kasumba moja ambayo tuko nayo sisi vijana na kasumba hiyo ni kujiona wewe bado ni mchanga hivyo huwezi kufanya jambo fulani katika hilo
    Bado mimi ni mdogo, nahitaji kumaliza kwanza chuo kisha nipate kazi nzuri na maisha mazuri,
Hakika hapo ndipo unajifunga kitanzi peke yako na utakufa bila kusaidika hasilani. Muda sahihi wakufanya kweli ni sasa. Kama ukiwa unangojea muda sahihi wa kuamua, kaa ukijua kua huo muda hautokaa uje na mwisho wa siku utaishia kuhangaika tuu.
      Chukulia mfano ningekua na fikra yakua wakati naanzasha blog hii ningesema huu sio muda sahihi wa kufanya hivyo eti tuu sababu niko chuoni nikisoma mambo ya Medical, leo hii nisingehesabu mafanikio yangu leo hii kwa kiburi. Niliamua kufanya hivyo sababu Idea nlikua nayo na niliamini muda pekee nilio kuwa nao kufanya hivyo ni ule nlioanzisha blog hii.All I’m saying is to start taking your dream seriously.TODAY.
Andika mambo yote unayo amini kua utayafanyia kazi na kupata mafanikio na kisha anza sasa kuyafanyia kazi. 
Fikiri kua ndio umenza na ndio uko katika ndoto zako na kisha weka nia juu ya hilo.
Japo wapo wengi wanafanya kile unachotaka kufanya lakini isikupe shida cha msingi wewe do it better
 Point ya mwisho ambayo ni 'do it better' ndiyo point niliyoamini nakuanza nayo. Ziko blog nyingi mno zenye wafuasi wengi lakini 'SIKUOGOPA' nilifanya kwa uzuri 'do it better' leo hii naweza kusimama nakufanya ama kuandika jambo na nikakubalika.

If they made it, why couldn’t I? And if I made it, why can’t you?



4: KUFUKIRI YAKUA HUNA CHAGUZIchase your dreams, why people don't chase their dreamsHapa inabidi niwe mbabe kidogo, Siku moja nilikua nikimweleza rafiki yangu juu ya ndoto zangu na akawa akinikejeli Sababu tuu yeye alikua teyari ana nyumba, gari na baadhi ya mali alizokua teyari akizimiliki. Sikumshangaa maana nilitambua kuachana mali alizokua akimiliki na hatua ambayo yeye alijiona keshapiga, lakini alikua amekosa baadhi ya vitu ambavyo mimi nilikua navyo na yeye hana vitu hivyo. Alikosa UHURU.
 Nilikua na uhuru wa :-
1.Kuchagua 
2.Uhuru wakufanya chochote ninachokitaka katika maisha yangu
3.Uhuru wakufanya makosa na kujutia.
Mwisho wa siku aliniambia "Una bahata samahani" nami nkamwambia sina bahati eti sababu tuu nina utofauti huo this life didn’t knock on my door, begging me to choose it.
I CHOSE TO CHANGE. AND SO CAN YOU: YOU DO HAVE A CHOICE. EVERY SINGLE DAY
Labda uwe Gerezani ama uwe mgonjwa mahututi, hakuna  Sababu yeyote inayokufanya usibadili maisha yako leo hiii kama kweli unataka kufanikiwa. Wako walemavu wengi wanaotembea na viti vya magurudumi lakini wanaizunguka dunia, hata vipofu nao hufanya hivyo je ni kwa nn wewe usifanye hivyo?
 If you think you don’t have a choice, think again. Is anyone forcing you to live your  current life?
Haijalishi watu walingojea nn kutoka kwako na wewe ukaona ni vyema kuwafuata ushauri wao ili kutokuwakwaza lakini unaamua kufanyab hivyo na ukawaridhisha lakini wewe utakua umemkwaza mtu mmoja katika maisha yako ambae ni .....WEWE
 Your person and your time are the most important assets that you will ever have. You can do incredible things with your life. No matter what your age is, it’s really never too late to choose a life that really suits you, and screw all those annoying people who try to convince you otherwise!

AND ALWAYS REMEMBER: “IF YOUR DREAMS DON’T SCARE YOU, THEY ARE NOT BIG ENOUGH” :)

Nichukue nafasi hii kukushukuru wewe ulietumia muda wako kusoma Uandishi huu kwa kua tuu umeamua kubadili mfumo wa maisha yako na kuachana na vifungo ulivyokua navyo'.
Tafadhali  Niandikie maoni yako hapo chini ama kama unataka kuzungumza nami nipiigie simu nambari 0767322193 na pia unaweza kunitumia barua pepe mtokambali2015@gmail.com
Ubarikiwe tena na tena.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...