08 December, 2015

Kongozi mmoja wa kundi la Al Shabaab ameuawa katika shambulizi la ndege ya Marekani

post-feature-image
Msemaji wa makao makuu ya ulinzi ya Marekani ,Peter Cook , kifo cha Abdirahman Sandhere ni pigo kubwa kwa usimamizi na uwezo wa mashambulizi ya kundi hilo linalounga mkono wanamgambo wa Al Qaeda.

Sandhere, anayejulikana pia kama " Ukash'' anadaiwa kuuawa Jumatano iliyopita. Al Shabaab inaendesha kampeini ya kuing'oa madarakani serikali inayoungwa mkono na jamii ya kimataifa ilikilindwa na zaidi ya majeshi 22,000 wa umoja wa Afrika. Kundi hilo limedhibitiwa katika maeneo mengi iliyokuwa ikikalia.

Hata hivyo kuwepo kwake na tishio la amani imedhihirika kupitia mashambulizi ya kigaidi mjini Mogadishu na vilevile katika taifa jirani la Kenya ambapo wapiganaji wake wametekeleza mashambulizi chungu nzima na kusababisha maafa makubwa.

Kwa mujibu wa duru za ujasusi za Marekani Al Shabaab inakabiliwa na changamoto kwa sababu ya ushawishi mkubwa wa Islamic State na Al Qaeda. Marekani imekuwa ikitekeleza mashambulizi ya ndege zisizokuwa na rubani kuanzia mwaka wa 2011.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...